jukwa la Wanainchi

Kalishi Tesha wa Tanga, Tanzania unasema, kuna msemo wa Kiswahili,’ vijana ni taifa la kesho’. Usemi huu sio sahihi hata kidogo. Kwani vijana wanatakiwa wajumuishe katika sera na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Lakini kwaq sasa kuna msukumo kiasi katika kuendeleza vijana, kwani baadhi ya mataifa yanayotoa elimu ya msingi bure kwa vijana.

Mfano nchini Tanzania kulikuwa na program ya kuendeleza shule msingi. Madrasa yamejengwa na idadi ya wanafunzi imeongezeka wanaohitimu shule ya msingi.

Pia kuna mpango wa kuendeleza shule za sekondari. Lakini program hii inakabiliwa na changamoto. Wanainchi wanahamu kubwa kujenga shule za sekondari za kata. Lakini kuna tatizo lakuwapata waalimu wenye sifa, pamoja na vifaa vya maabara kwajili ya masomo ya sayansi.

Naye Daudi Pikikoti kutoka hospitali ya mkoa Iringa, Tanzania anasema tupo katika dunia ambayo muumbe ametuweka tuishi watu na viumbe mbalimbali wanaondelea kuishi kilamoja kadre anavyoweza. Dunia ambayo hauishi matatizo. Dunia iliyo kosa amani. Ukiangalia kulia, ndugu jamaa na marafiki, wako wodoni wamelazwa. Wakati huo huo zinahitajika fedha kwa ajili ya matibabu.

Ukiangalia kushoto, vita na mauaji, pamoja na matetemeko bila kusahau maafriko yakunusuisha. Ukigeuka nyuma umaskini wa kipato unanizunguka. Mwanadamu, kila ninacho fanya hakilipi. nikiangalia mbele, hakuna matumaini ya kuishi raha mstarehe. Oh, ole wangu mimi mwanadamu, ni nani atakaye niokowa na matatizo haya? Eh, mola muumba wa dunia, na muumbaji wetu, wewe tu unaweza kutuokowa na matatizo haya? Fanya haraka kutu saidia tunaongamia. 



_TTEXT2ALT_
What is this? Print Page Close Window
Close About
The source is the authentic content from which this lesson was developed. The source can prove extremely useful for learners. You can review authentic materials with total confidence that the materials are at the indicated level. You can easily check your overall comprehension of the materials by simply reading the provided translation. Lastly, you can listen to the authentic audio to check the pronunciation of words or phrases.